Miongo mitano baada ya misheni ya mwisho ya Apollo, Mwezi kwa mara nyingine tena uko kwenye njia panda za uchunguzi wa anga. Kwa sasa sio NASA pekee inayovutiwa au inayoweza kufanya uchunguzi wa mwezi.
Idadi ya wanaanga
waliotembea Mwezini imekuwa ileile kwa zaidi ya miaka 50, ni watu 12 tu ndio
wamepata fursa hiyo na wote ni Wamarekani. Lakini hiyo inakaribia kubadilika.
Serikali na
makampuni ya kibiashara kutoka Ulaya na Mashariki ya Kati hadi Pasifiki Kusini
wanazindua ujumbe wa kuzunguka Mwezi au kutua juu ya uso wake.
Mashindano ya
kihistoria kati ya mashirika ya anga ya juu ya Amerika na Usovieti kwa
uchunguzi wa mwezi yamekuwa ya kimataifa.
Licha ya mafanikio
ya ujumbe wa Apollo wa Marekani kati ya mwaka 1969 na 1972, hadi sasa ni
mataifa matano pekee ambayo yametua mwezini.
Baada ya safari
mbili za kuuzunguka mwezi zilizofaulu mnamo 2007 na 2010, Uchina ilitua chombo
cha Chang'e 3 isiyo na rubani mwezini mnamo 2013.
Miaka sita baadaye,
Chang'e 4 ikawa ujumbe wa kwanza kutua upande wa mbali wa Mwezi.
Roboti ya Chang'e 5
ilirejesha sampuli za mwezi duniani mwaka wa 2020 na Chang'e 6, iliyozinduliwa
Mei mwaka huu, italeta sampuli za kwanza kutoka upande wa mbali wa Mwezi.
Na mipango ya nchi
ya Asia haiishii hapo.
0 Comments:
Post a Comment