LAZARO NYALANDU-KILA MWENYE KADI YA KUPIGA KURA HAKIKISHA OCTOBER 29 MAPEMA UNATIKI

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu, amewaomba wananchi kila mwenye kadi ya kupiga kura kuhakikisha anaitumia kadi hiyo kutiki ili kuwapata viongozi wanakao jibu changamoto zao.

Nyarandu amesema chama kilichobeba maono ya nchi na chenyeuwezo wa kutatua changamoto za wananchi ni CCM pekee hivyo wananchi wanaowajibu wa kuhakikisha wanakipatia chama hicho kura zakutosha.

Akizungumza kuhusu mkoa wa Singida kila mwananchama wa chama cha Mapinduzi anaowajibu wa kuulinda Mkoa wa Singida kwa kumpigia kura nyingi kwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan,wagombea ubunge pamoja na udiwani.

Nyalandu amesema hayo wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Ilongero Haidery Gulamali uliofanyika kata ya Mtinko.

Amesema Mkoa wa Singida ambao ni wa CCM ni lazima uchaguzi wa mwaka huu uongoze kwa kura za kishindo kwa wagombea wote wa CCM.

"Nitasimama pamoja na mgombea ubunge jimbo la Ilongero,Gulamali na kuhakikisha mama Samia Suluhu Hassan anapata kura zote,tunataka watu wote watoke kupiga kura.

Amesema anaungana na timu ya kitaifa kwa kutembelea kila mkoa ili kuhakikisha CCM inapata kura nyingi za kutosha kuanzia kwa mgombea Urais,Wabunge pamoja na Madiwani.

Aidha, Nyalandu katika kuhakikisha madiwani hawakwami katika Kampeni alitoa shilingi milioni 15 kwa madiwani 21 wa kata na madiwani 9 wa viti maalum ili waweze kupiga kampeni vizuri na kufika kila kata,kijiji na kitongoji kusaka kura za CCM.




 

About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment