SINGIDA MILANGO YA UWEKEZAJI IKO WAZI




 Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga akiwa katika mazungumzo na wageni kutoka nje ya nchi waliofika kwa nia ya kupata miongozo na fursa ya maeneo ya uwekezaji Mkoani Singida amewahakikishia kuwa Singida ni mahali salama kwa uwekezaji.

Katika majadiliano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ukishirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Singida,Maafisa biashara kadhalika Mameneja wa Taasisi,Wawekezaji wamepata kuelezwa taratibu mbalimbali za kufuata ili waweze kupata fursa hiyo. 

Kadhalika,Dkt. Fatuma Mganga ameeleza kuwa Mkoa wa Singida unawakaribisha Wawekezaji katika sekta zote zilizo ainishwa kwa kipaumbele na Serikali katika nyanja zote, na kuahidi Ushirikiano katika kuhakikisha Mkoa wa Singida unapata Maendeleo yatokanayo na uwekezaji huo.

Amesema Mkoa wa Singida Milango ipo wazi kuwapokea wawekezaji kwa kufuata taratibu zote na vipaumbele vya Mkoa wa ili wananchi waweze kunufaika na uwekezaji huo.

Amesema zipo fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya Kilimo,Madini,Afya,Elimu pamoja na yingine nyingi ikiwemo mawasiliano.



About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment