SHIRIKA LA PATRONAGE CENTER FOR PERSONS WITH DISABILITY (PPD) KUTEKELEZA MRADI WA SAUTI ZETU

SINGIDA

Shirika lisilokuwa la Kiserikali ambalo linafanya kazi bila kutengeneza faida,lenye malengo ya kutetea haki za watu wenye ulemavu la lenye makao yake makuu mkoania Singida  la PATRONAGE CENTER FOR PERSONS WITH DISABILITY (PPD) linatekeleza Mradi wa sauti zetu wenye lengo la kuwafikia vijana katika manispaa ya Singida.

Mradi huo wa SAUTI ZA ZETU unafadhiliwa na Shirika la STICTING OXFAM NOVIB kwa thamani ya wa EUR 20,000.00.

Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika hilo la PPD Bw, Mauridi Ramadhani Mrisho amesema Mradi huo unalenga vijana wenye ulemavu, ukiwa na dhumuni la kuwapatia fursa sawa za kielimu, kijamii na kiuchumi,vijana ambao mara nyingi hukumbana na changamoto za kutojumuishwa ipasavyo katika jamii, jambo linalozuia ndoto na vipaji vyao kustawi. 

‘‘Lengo kuu ni kuhakikisha vijana wenye ulemavu wanapata nafasi za usawa katika elimu,ajira na ujasiriamali. Pia, tunataka kuongeza uelewa kwa jamii ili kupunguza unyanyapaa na vikwazo vya kijamii vinavyowakabili’’ 

Kwa kufanya hivyo, tunapanua wigo wa ushiriki wao kikamilifu katika maendeleo ya taifa’’Amesema Mauridi.

 Aidha amesema Kupitia mradi huo, vijana wenye ulemavu watapata nafasi ya kujitegemea kiuchumi, kuongeza kujiamini, na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii huku jamii itanufaika kwa kupunguza utegemezi, na kukuza mshikamano wa kijamii unaoheshimu tofauti na usawa.

Amesema tayari wamemaliza kuwajenga uwezo wafanyakazi wa ofisi hiyo utakao wawezesha kutekeleza mradi huo kwa ufanisi zaidi.

 Katika hatua nyingine Bw Mrisho amezengumzia malengo mahususi ya Shirika hilo kuwa nipamoja na Shirika kuelimisha  na kufahamisha kuhusu haki na utu wa watu wenye ulemavu  kuwawezesha   wanawake wenye ulemavu kisiasa, Kiuchumi na kijamii,kutetea kwa usawa fursa za watu wenye ulemavu kwa kuzingatia maamuzi na nafasi zao pamoja na kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa kwenye miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kutoa mchango wao kuhakikisha kuwa dunia inakuwa mahali salama.

Kwa jumla, mradi wa vijana wenye ulemavu ni chachu ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Unatoa mwanga wa matumaini kwa vijana hawa na unajenga jamii yenye mshikamano, usawa na heshima kwa utu wa kila mmoja. Kupitia mradi huu, dhana ya “ulemavu siyo kikwazo” itadhihirika kwa vitendo.

  


Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika hilo la PPD Bw, Mauridi Ramadhani Mrisho akipokea cheti
Tuzo ya heshima iliyotolewa na mbunge wa viti maalumu Neema Lugangira kwa PPD kutambua umuhimu wa shirika hilo




 

About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

1 Comments: