Kenya imewaondolea ada ya kuingia nchini himo wamiliki wa paspoti za kusafiria kutoka Afrika Kusini na nchi nyingine sita bada ya ada hiyo kuanzishwa mwezi uliopita .
Serikali ilitupilia
mbali mahitaji ya viza kwa wamiliki wote wa pasipoti za kigeni mwezi uliopita.
Hatua hiyo
ilionekana kama jaribio la kuitangaza Kenya kama kivutio cha utalii na kuvutia
wasafiri wa kibiashara.
Lakini ada ya
kuingia ya $30 (£23) ilianzishwa, ikijumuisha kwa baadhi ya wageni ambao hapo
awali hawakuhitaji visa.
Uamuzi huo ulizua
msukosuko mkubwa, huku wakosoaji wakisema kuwa huenda ukasababisha nchi ambazo
Kenya ina mikataba ya kuondoa viza kuanzisha ada sawa na hiyo, hivyo kufanya
usafiri kuwa wa gharama kubwa .
Ni wasafiri tu
kutoka jumuiya ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao
hawakuruhusiwa kulipa pesa hizo.
Mbali na Afrika
Kusini, msamaha huo umeongezwa kwa wamiliki wa pasipoti kutoka mataifa mengine
matano ya Afrika - Ethiopia, Eritrea, Congo-Brazzaville, Comoro na Msumbiji.
San Marino, taifa la
tatu kwa udogo barani Ulaya, ndiyo nchi nyingine pekee kwenye orodha ya
kutotozwa ada.
Taarifa kutoka kwa
wizara ya mambo ya ndani ya Kenya na idara ya uhamiaji ilisema nchi
zisizohitajika kulipa ada hiyo zimeingia "mkataba wa kukomesha visa au
kutia saini makubaliano ya pande mbili ya kuondoa visa" na taifa hilo la
Afrika Mashariki.
Hata hivyo, wasafiri
kutoka nchi hizi bado watahitaji kupata hati ya uidhinishaji wa usafiri wa
kielektroniki (ETA) mapema ili kuingia Kenya, na kuwasilisha maelezo kama vile
maelezo ya ndege na uthibitisho wa mahali pa kulala.
ETA ni idhini ya kuingia mara moja nchini na ni halali kwa siku 90.
0 Comments:
Post a Comment