RUFIJI.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Luteni Kanali Fredric Komba amewataka Vijana wa JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Nishati Safi waliomaliza mafunzo ya JKT katika Kikosi cha Kibiti JKT kilichopo mkoani Pwani kubeba ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya matumizi ya Nishati safi katika Jamii kama walivyopewa heshima ya Jina la Operesheni yao.
Mhe. Luteni Kanali Komba, ameyasema hayo leo Septemba 18,2025 wakati wa sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Vijana wa Mujibu wa Sheria kikosini hapo
Aidha, Mhe. Komba amewataka Vijana wahitimu wa mafunzo hayo kuwa mabalozi Wazuri katika Jamii kuhusu Ulinzi na Usalama wa nchi kwani wao ni Jeshi la akiba.




0 Comments:
Post a Comment