WAJUMBE WA BODI YA SUWASA SINGIDA WATEMBELEA MAENEO YA HUDUMA YA IKUNGI NA PUMA

 

SINGIDA 

Wajumbe wa Bodi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) wametembelea maeneo ya kihuduma ya Ikungi na Puma ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kukagua hali ya huduma ya Maji kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya SUWASA Bw. Kitila Mkumbo na kuhusisha Wajumbe wa Bodi na Watendaji wa Mamlaka. 

Wajumbe hao walipata fursa ya kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Tom Apson ambaye katika maelezo yake alieleza kuwa Serikali ya Wilaya inaridhishwa sana na utendaji kazi wa SUWASA Ikungi na kwamba tangu wamekabidhiwa Ikungi, SUWASA imefanya kazi kubwa ya maboresho ya huduma ya Maji ambapo kwa sasa hali ya upatikanaji Maji imekuwa Bora zaidi ikilinganishwa na kabla SUWASA kukabidhiwa eneo hilo la Ikungi mjini. 

"Mwanzoni tulikuwa hatuna imani kabisa na SUWASA kukabidhiwa eneo hili kulihudumia lakini muda ulipokuwa unaenda SUWASA imefanya kazi kubwa ya kuboresha huduma ya Maji Ikungi mjini na yale malalamiko kwa sasa hakuna", alieleza Mkuu wa Wilaya.

Aidha, Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi alieleza kuwa katika siku za mbeleni Serikali ione uwezekano wa kuikabidhi SUWASA maeneo zaidi ya Ikungi ambayo yanageuka kuwa miji kwani uwezo wa kiutendaji wa SUWASA ni mzuri. 

Katika ziara hiyo, Wajumbe wa Bodi walitembelea pia matenki mawili ambayo yalikuwa yanavuja na kusababisha upotevu mkubwa wa Maji na kwa sasa hayavuji na yameongeza upatikanaji Maji kwa Wananchi.

Pia Wajumbe wa Bodi walitembelea ofisi ndogo ya SUWASA Ikungi na kuongea na Watumishi pamoja na ofisi ndogo ya PUMA.

Wajumbe wa kamati wakiwa katika picha ya pamoja.

MKUU WA WILAYA YA IKUNGI MKOAN SINGIDA 

MENEJA WA SUWASA SINGIDA 




About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment