NA
Kitengo cha habari serikalini mkoa Singida
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Iramba imetoa Semina ya Siku Moja kuhusu Elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, Kwa Makundi ya Watu wenye Mahitaji Maalumu.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TAKUKURU Wilaya ya Iramba yametolewa Januari 27, 2025 katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na kuwashirikisha baadhi ya wawakilishi kutoka Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) ,Chama Cha Watu Wasiiona (TLB), Chama Cha Walemavu wa Viungo ( CHAWATA ), Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA)
Akizungumza katika kuhitimisha mafunzo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Bi. Bupe Mwakibete amewataka wawakilishi hao kutoka vyama vya Watu wenye Mahitaji Maalumu kuendelea kutoa Elimu kwa wenzao juu ya mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu la Kila mtu hivyo kutoa ushirikiano pindi wataksoohitajika kufanya hivyo
"Jukumu la Mapambano ya Rushwa ni letu sote,tuhakikishe tunakuwa mstari wa mbele dhidi ya mapambano haya kuelekea kipindi hiki Cha Uchaguzi. " Amesema DAS Bupe Mwakibete.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania Bw. Nassoro Ernest Amos ameishukuru TAKUKURU kwa kutoa Mafunzo hayo kuhusu Elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 kwa Makundi ya watu wenye Mahitaji Maalumu kwani wamepata Elimu itakayowawezesha kuwa mstari wa mbele kushiriki Katika mapambano dhidi ya Rushwa
"Tumepata Elimu itakayotuwezesha na sisi watu wenye Mahitaji Maalumu kushiriki Katika mapambano hayo kwa kuwa Rushwa ni adui mkubwa wa haki na wajibu wetu ni kuitokomeza kwa kuhakikisha tunachagua Viongozi Waadilifu ambao hawajatokana na Rushwa" Alisisitiza Nassoro Amos
NA,Kitengo cha habari serikalini mkoa Singid.
0 Comments:
Post a Comment