Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini Malawi limemkosoa vikali Rais Lazarus Chakwera wa nchi hiyo na kueleza kwamba, utawala wake umefeli na hujawa na mafanikio kwa wananchi.
Taarifa ya maaskofu wa Kanisa Katoliki nchinii Malawi imeeleza kuwa, nchi imekuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
Katika kauli nzito inayoonekana kuelekezwa kwa rais, kanisa hilo kupitia maaskofu wake lilisema "tumeshuhudia kufeli kwa uongozi".
"Raia wa Malawi hawaoni mtu yeyote katika serikali ya sasa anayewajali au ambaye anaweza kuboresha hali zao," iliongeza taarifa hiyo.
Waraka wa wachungaji wenye kurasa 16 wenye kichwa "Hadithi ya kusikitisha ya Malawi", ambao ulisomwa katika makanisa yote ya Kikatoliki nchini kote siku ya Jumapili, ulishutumu uongozi wa Rais Chakwera kwa kushindwa kwa kiasi kikubwa kutekelezwa ahadi za kampeni, kuweko upendeleo wa kindugu na ufisadi uliokithiri nchini humo.
Kwacha, sarafu rasmi ya MalawiKanisa hilo linashutumu serikali ya Rais Chakwera kwa kupendelea watu wa kabila au eneo fulani inapowateua watu kwenye nyadhifa za juu na kuwadhulumu wanahabari wanaofichua ufisadi.
Sehemu nyingine ya waraka huo pia ilisema kuwa, serikali imeshindwa kuinua kipato cha watu hata baada thamani ya sarafu ya Malawi kushuka kwa kiasi kikubwa.
Novemba mwaka jana (2023) Rais wa Malawi aliitangaza kusitisha safari zake zote za nje ya nchi, yeye na maafisa wa serikali wakiwemo mawaziri kama sewhemu ya kubana matumizii.
Malawi inapambana na mgogoro wa kiuchumi ambao umesababisha uhaba wa mafuta, kupanda bei za vyakula na uhaba wa fedha za kigeni.
0 Comments:
Post a Comment