Mtu mmoja ameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israel kwenye nyumba moja kusini mwa Lebanon.
Watu wengine zaidi ya saba wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.Kulingana na vyanzo vya usalama vya Lebanon raia aliyeuwawa ni mwanamke na miongoni mwa waliojeruhiwa ni watoto.
Hata
hivyo jeshi la Israel limesema linachunguza ripoti hiyo iliyotolewa na Shirika
la Habari la Taifa la Lebanon.
Shambulizi
la Israel limejiri baada ya Hezbollah inayoungwa
mkono na Iran kudai kuhusika na mfululizo wa mashambulizi ya roketi na ndege
zisizo na rubani kwenye vituo vya kijeshi vya Israel upande wa kaskazini.
Haya
yanajiri huku wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema watu 37,266
wameuawa katika ukanda huo katika vita vilivyodumu kwa zaidi ya miezi minane
kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.
0 Comments:
Post a Comment