MWANDISHI WA HABARI WA RADIO FREE AFUNGWA GEREZANI RUSSIA


 Mahakama moja ya Russia imemtia hatiani Alsu Kurmasheva, mwandishi wa habari mwenye asili ya Russia aliyekuwa akifanya kazi kwenye Radio Free Europe/Radio Liberty inyofadhiliwa na serikali ya Marekani.


Mwandishi huyo wa habari alituhumiwa kwa kusambaza habari za uongo kuhusu jeshi ya Russia na kuhukumiwa miaka sita na nusu gerezani kufuatia kesi hiyo ya siri, rekodi za mahakama na maafisa walisema Jumatatu.


Hukumu hiyo ilitolewa huko Kazan, mji mkuu wa mkoa wa Tatarstan wa Russia ulioko katikati, alikuja siku ya Ijumaa, siku hiyo ambayo mahakama ya jiji la Yekaterinburg huko Russia ilimtia hatiani mwandishi wa Wall Street Journal Evan Gershkovich kwa tuhuma za ujasusi na kumuhukumu miaka 16 jela, kesi ambayo Marekani inaiita kuwa ni ya kisiasa.


Kurmasheva, mwenye umri wa miaka 47- mhariri wa RFE/RL, idhaa ya lugha ya Tatar-Bashkir, amehukumiwa kwa “kusambaza habari za uongo” kuhusu jeshi, kulingana na tovuti ya mahakama kuu ya Tatarstan. Msemaji wa mahakama Natalya Loseva alidhibitisha hukumu ya Kurmasheva na kuifichua hukumu hiyo kwa shirika la habari la Associated Press kwa njia ya simu katika kesi hiyo inayoainishwa kuwa ya siri.


Alisema mwaka jana mashitaka hayo yalitokana na kitabu cha Idhaa ya Tatar-Bashkir kilichotolewa mwaka 2022 kikiitwa “Hapana Vita” —“ mkusanyiko wa hadithi fupi za Warussia ambao hawataki nchi yao kuwa vitani na Ukraine.”


Alipoulizwa kuhusu kesi hiyo, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa RFE/RL Stephen Capus aliishitumu kesi hiyo na kuhukumiwa kwa Kurmasheva kuwa kama “dhihaka ya haki

About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment