Saabu ya kwanza ya kuishi muda mfupi duniani
ni kutokumtumikia Mungu. Kuishi muda mrefu ni moja ya Baraka za Mungu, Mungu
anapombariki mtu anampa afya, anampa mali, anambariki pamoja na nyumba yake,
anampa uzima wa mille, anambariki na kizazi chake chote.
Kutoka 23:
Kila mtu amepangiwa hesabu ya siku zake za
kuishi hapa duniani. Inaweza kuwa miaka 70 au zaidi ya 80. Ukimtumikia Mungu
atakuheshimu na hesabu ya siku zako za kuishi ataitimiza. Tunayo kampeni ya
kuishi muda mrefu kwa kumtumikia Bwana, tunawaombea watu, tunatoa pepo na
kuponya magonjwa, tunafufua wafu, tunafungua watu, tunafanya mikutano kwa nguvu
zetu zote kwasababu tunamtumikia Bwana ili tuishi muda mrefu na kupokea Baraka
zake.
Watu wa dunia hii wakikupa kidogo utalipia,
mfano umeme unapewa uwashe usiku lakini unalipia fedha nyingi ukiangalia Mungu
anatuangazia Asubuhi mpaka jioni na usiku na hatulipii chochote, angalia pumzi
ya Mungu matajiri na maskini wanavuta kwa kiwango sawa, wenye dhambi na wasio
na dhambi wanavuta pumzi ya Mungu kwa pamoja. Kalebu alikua anamtumikia Bwana
Akamzidishia miaka ya kuishi. Kama wewe unamtumikia Bwana. Ukimtumikia Bwana
hautaishi muda mfupi hapa duniani utaishi muda mrefu kwa jina la Yesu.
Sababu ya Pili kwanini watu wanakufa mapema
ni dhambi, kila unapoona kifo ujue dhambi ilikuwepo pale kabla. Nyuma ya kifo
kuna mauti, Biblia inasema tama ikishakuchukua mimba inazaa dhambi na dhambi
ikishakukomaa huzaa mauti.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni
mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Duniani kote mishahara inabadilika na kuyumba
lakini mshahara wa dhambi haujayumba umebaki vilevile. Mshahara wa dhambi ni
mauti lakini karama ya Mungu ni uzima wa milele.
1 Yohana 5:20 “Nasi twajua kwamba Mwana wa
Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,
nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu
Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.”
Yohana 3:18 “Amwaminiye yeye hahukumiwi;
asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa
Mungu”.
Dhambi itakufanya ufe kabla ya wakati.
Unatenda dhambi kwa siri hakuna mtu anajua lakini ukfa kila mtu atakuona
waziwazi.
Ezekieli 18:3-5 “Kama mimi niishivyo, asema
Bwana MUNGU, hamtakuwa na sababu ya kuitumia tena mithali hii katika Israeli.
Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo
ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa. Bali kama
mtu ni mwenye haki, na kuyatenda yaliyo halali na haki;”
Jambo la tatu linaloleta kifo kabla ya wakati
ni kutokulishika neno la Mungu.
Mithali 4:20-22 “Mwanangu, sikiliza maneno
yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako;
Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya
mwili wao wote.”
Kwakadiri unavyoweka neno la Mungu ndani
yako, Neno la mungu linakupa afya na Uhai Yesu atakuja kwako atafanya makao
kwako. Kama umeokoka unaishi maisha ya kumcha Mungu hufi mpaka wewe umesema
‘Bwana naomba nipumzike’. Hata wale wanaosema ‘simwogopi mtu nipo tayari kwa
lolote hata kufa, wanasema vile inakua tayari wamesaini cheti cha kufa, mwana
ume wa kweli anasema simwogopi mtu na sifi nasema leo na nitasema tena’
Sababu ya Kutokuwa na Neno la Mungu.
Ikitokea umekosea Mwombe Mungu msahama kama
ilivyoandikwa 1 Yohana 1:9, Zaburi 103:3, Zaburi 107:12, Isaya 1:18, Isaya 45
Sisi tuliokolewa tuna agano na Bwana ndiomaana tukikosea tunasamehewa.
Sababu nyingine ya kuishi muda mrefu ni
kuwatii Baba na Mama.
Waefeso 6:1-4 “Enyi watoto, watiini wazazi
wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri
hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na
maonyo ya Bwana.”
Hii ni amri ya kwanza yenye ahadi, hapa kuna
wazazi wa aina mbili Maana yake enyi watoto watiini wale waliowazaa katika
Bwana na wazazi wa kimwili . Watumishi wa Mungu wametuzaa kiroho. Biblia
inasema watiini wazazi wenu katika Bwana, tukifanya hivyo tutaishi miaka mingi
Elisha alimtii Eliya ambaye alikua mzazi wake wa kiroho akaishi muda mrefu,
mstari wa pili unaongelea kwa wazazi wa kimwili. Ukiwaheshimu wazazi wa kiroho
na kimwili utaishi miaka mingi hapa duniani.
Kuna aina mbili za kifo, aina mbili za kifo,
aina ya kwanza ni wale ambao hawajazaliwa mara ya pili(kuokoka) na aina
nyingine ni kile kifo cha jehanamu. Mzazi anaweza kuwa mlevi lakini bad ni ni
mzazi huwezi kumkataa.
Sababu nyingine inayomfanya mtu aishi muda
mfupi ni kukimbia kwa kasi, kila mtu ananafasi yake kufanya kazi duniani.
Ukifanya kazi yako kwa nguvu sana ukamaliza mapema sana Mungu anaamua
akupumzishe kwake ili usije ukakaa muda mrefu duniani ukasababisha matatizo.
Mkumbuke Ezekia aliishi akamuomba Mungu akamwongezea miaka kumi na mitano baada
ya kumaliza kazi yake. Ukisoma Kwenye Biblia ile miaka aliyoongezewa alifanya
mambo mabaya sana.
Kuna nchi ipo mbinguni na Raisi wake ni Bwana
Yesu ambaye hapa tunamwona kwenye Neno lake lakini mbinguni kule tutamwona
jinsi alivyo. Mfano Yesu kristo alikufa akiwa na miaka 33 tu na aliifanya kazi
yake ndani ya miaka mitatu na nusu pekee. Alikua anaamka saa 11, asubuhi
anapanda mlimani kuomba baadae anateremka asubuhi anapiga mikutano na jioni
anarudi mlimani kuomba kesho yake tena na tena na tena mpaka akamaliza kazi
akafa akiwa na miaka 30+ . Ukimaliza kazi yako Mungu anakuchukua kama Henoko au
Eliya nabii ambao walitwaliwa (simaanishi ufanye kazi kwa ulegevu hapana!)
usiishiwe kazi ya ufanya kwaajili ya Mungu. Ukimaliza kazi halafu ukamwomba Mungu
akupe miaka mingine utajikuta umefanya mambo mabaya sababu umeshamaliza kazi
yako.
Sababu ya Sita ni kutokufanya mazoezi. Biblia
inasema mazoezi ya mwili yafaa kidogo na mazoezi ya kiroho yafaa sana. Mazoezi
yanamfanya mtua aishi muda mrefu. Mwanadamu hakuumbwa ili aendeshe gari, Gari
halikua kwenye mawazo wa Mungu, mwanadamu aliumbwa kazi yake ilikua kuishi
bustani ya Eden kazi yake ilikua ni kuzunguka ili ale, mwanadamu alipokosea
Mungu alimwambia atakula kwa jasho lake, Mwanadamu akaamua kutengeneza mashine
ili arahishishe kazi. Kama hufanyi mazoezi ukiwa mzee utasumbuka sana.
Sababu nyingine ni madawa, kuna watu wengine
kichwa kidogo wanakunywa dawa, watu wengi wanakunywa dawa sana ambazo
zinawafanya wawe viziwi na kuharibu miili yao. Kuna vidonge ambazo wanawake
wanameza kila siku matokeo yake vinawaletea matatizo (Yesu ninuponyaji tosha).
Namna nzuri ni kutumia tamaduni za asili kuangalia ni tarehe zipi mama anaweza
kupatwa na ujauzito. Kila mtu aangalie kwa makini sana, unaweza ukajikuta
unaishi muda mfupi sio kwasababu hulishiki neno la Mungu bali ni kwasababu ya
madawa unayokula kila siku.
Haya ni mambo yanaweza kumfanya mtu aishi
muda mfupi au mrefu. Ukipata tatizo angalia ni eneo lipi ulilokua mlegevu
usimame tena
0 Comments:
Post a Comment