Matokeo ya kura ya mchujo iliyofanyika siku ya
Jumanne kwenye zaidi ya majimbo 15 ya Marekani yanaendelea kutolewa huku Rais
Joe Biden na mpinzani wake Rais wa zamani Donald Trump wakijizolea ushindi wa
majimbo mengi.
Kura hiyo ya mchujo ndiyo itakayoamua wanasiasa watakaopeperusha
bendera ya vyama vikuu viwili katika uchaguzi wa rais nchini Marekani
utakaofanyika mwezi Novemba.
Rais Joe Biden kutoka chama cha Democratic anawania muhula wa
pili bila ushindani wowote mkubwa na inatazamiwa ndiye atakuwa mgombea wa chama
hicho.
Kwa upande wa Republican, rais wa zamani wa Marekani, Donald
Trump ndiye anapigiwa upatu wa kuwa tena mgombea, katika kile kinatazamwa
kuwa uwekano wa mpambano mwingine kati yake na Biden aliyemshinda mwaka 2020.
Hadi mapema asubuhi, Biden tayari alikuwa ametangazwa mshindi
kwenye majimbo kadhaa yaliyoshiriki kura ya mchujo ya jana
Jumanne inayofahamika kama "Kinyang´anyiro cha Jumanne Kuu".
Biden ameshinda majimbo ya Oklahoma, Virginia, Tennesee, North
Carolina, Vermont na Iowa. Mengine ni Maine, Utah, Minnesota, Texas na
Massachusetts.
0 Comments:
Post a Comment