SINGIDA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amefungua Kliniki ya Utatuzi wa Kero za Walimu Mkoa wa Singida (Samia Teacher's Mobile Clinic), akiamini kuwa kutatuliwa kwa kero za walimu kutasaidia kuboresha mazingira yao ya kazi na kuongeza ubora katika ufundishaji.

Kliniki hiyo imefunguliwa katika Ukumbi wa Mabula Social Hall, Manispaa ya Singida, na inatarajiwa kutoa suluhu kwa changamoto zinazowakabili walimu katika mkoa huo.

Kliniki hiyo imeratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Utumishi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na Tume ya Utumishi wa Walimu.

Aidha Lengo kuu la kliniki hiyo ni kutatua kero za walimu na kuboresha mazingira yao ya kazi ambapo Walimu wenye kero kutoka Halmashauri saba za Mkoa wa Singida (Manispaa, Singida DC, Makalam, Itigi, Manyoni, Iramba na Ikungi) wakihudhuria.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Dendego amesisitiza kuwa lengo la kliniki ni kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa bidii na kujitolea licha ya changamoto zinazowakabili.

Amepongeza walimu kwa juhudi zao za kujituma katika ufundishaji.

Akizungumza makamu wa rais wa chama cha walimu Mwl Suleiman Ikomba amesema kliniki hiyo ni mwarobaini wa kutibu changamoto za walimu kote nchini.

Amesema Singida ni mkoa wa 14 tangu kuaza kwa kampeni hiyo na mikoa yote walikopita wamesikiliza na kutatua kero za walimu.

Makamu wa rais wa chama cha walimu Mwl Suleiman Ikomba

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amefungua Kliniki ya Utatuzi wa Kero za Walimu Mkoa wa Singida (Samia Teacher's Mobile Clinic)


About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment