SINGIDA
Na,Glory Izack
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Singida leo Februari 11,2025 wametoa elimu kwa viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa kimila,wazee maarufu,viongozi wa asasi zisizo za kiserikali na watu wenye mahitaji maalumu juu ya madhara ya rushwa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu 2025,mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi(NAO)mkoani Singida.
Awali akiwasilisha mada katika semina hiyo,Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU mkoani Singida, Bw.Joseph John Kailanya ametoa mada kuhusu aina za rushwa katika uchaguzi,makosa ya jinai katika katika uchaguzi na njia mbali mbali za kuripoti taarifa za vitendo vya rushwa na madhara ya rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Singida Bi.Sipha Mwanjala ameainisha majukumu ya Taasisi hiyo ambayo ni "KUZUIA NA KUPAMBANA"na rushwa kwa lengo la kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mmoja.Pia amewasisitiza wananchi kutumia jukwaa la 'TAKUKURU RAFIKI' ili kupata elimu kuhusu Masula ya rushwa na pia kuwawezesha kuibua kero mbalimbali na kupendekeza namna gani ya kuzitatua.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ambaye amekua mgeni rasmi katika semina hiyo amezungumzia kuhusu madhara ya rushwa katika uchaguzi akiainisha baadhi ya madhara yake hasi ikiwemo kuchagua viongozi wasiofaa katika jamii ambao hushindwa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi pamoja na kuharibu misingi ya demokrasia ambayo hupelekea kuharibu amani na uchumi wa jamii na nchi yetu kwa ujumla.
"Tunao wajibu wa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuiepuka rushwa hususani katika kipindi kijacho cha uchaguzi,ili kuwapata viongozi bora ni lazima tuikemee rushwa ili kudumisha haki na uwajibikaji wao kwa wananchi"amesema Mhe.Dendego.
Pia ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa TAKUKURU kwa wakati wowote watakapohitaji ushirikiano wao,pia kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatosha kwa lengo la kuhakikisha utendaji bora wa kazi na kwa haki kwa kuhakikisha wote watakaohusika katika vitendo hivyo wanachukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego na Mkuu wa TAKUKURU mkoani Singida Bi.Sipha Mwanjala
0 Comments:
Post a Comment