Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amewakemea hadharani maaskofu wa Ujerumani kuhusu mwongozo wa kutoa baraka kwa ndoa ya jinsia moja




Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amewakemea hadharani maaskofu wa Ujerumani kuhusu mwongozo unaowaruhusu wanandoa wa jinsia moja kupokea baraka za kanisa. 

Akizungumza wakati akiwa kwenye safari ya kurejea nyumbani kutoka ziara yake ya siku kadhaa barani Afrika, Leo alisema;

"Uongozi wa Kanisa tayari umezungumza na maaskofu wa Ujerumani na umeweka wazi kwamba haukubaliani na baraka rasmi ya wanandoa wa jinsia moja au wanandoa walio katika hali zisizo za kawaida zaidi ya kile ambacho Papa Francis aliruhusu kwa kusema watu wote wanapaswa kupokea Baraka."

Ametoa kauli hizo baada ya Askofu Mkuu wa Munich na Freising, Kardinali Reinhard Marx, mapema wiki hii kuidhinisha baraka za wanandoa wa jinsia moja katika dayosisi yake. 

Msimamo wa Marx ulitokana na mwongozo uliotolewa na Jumuiya ya Maaskofu wa Ujerumani na Kamati Kuu ya Wakatoliki nchini Ujerumani, ambao ulionekana kuwa sawa na maoni ya papa wa zamani Francis. 

Hata hivyo, mrithi wake, Leo, papa wa kwanza kutoka Marekani, anaaminika kuwa mhafidhina zaidi katika masuala ya kijamii.

Akiwa safarini kurudi nyumbani kutoka Guinea ya Ikweta, Leo aliwaambia waandishi wa habari kwamba "umoja au mgawanyiko havipaswi kuzunguka masuala ya ngono," akisisitiza "kuna masuala makubwa zaidi na muhimu zaidi kama vile haki, usawa, uhuru wa mwanaume na mwanamke, uhuru wa dini ambavyo vyote vinapaswa kupewa kipaumbele kabla ya suala hilo."




About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment