Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ameagiza Mgambo walioenda soko la Samunge Jijini humo na kuwafanyia fujo kisha kuwanyang’anya Wafanyabiashara vitu vyao, wakamatwe ndani ya saa 24 kuanzia wasa kisha wamtaje aliyewatuma kuwaonea Wafanyabiashara na pia Mgambo hao warudishe vitu vyote walivyochukua.
Akiongea Makonda ameagiza pia Msimamizi wa soko hilo asimamishwe kazi mara moja na Mamlaka iliyompa kazi na kisha uchunguzi uanze kufanyika ili kubaini kwanini soko hilo haliishi migogoro.
RC Makonda amesema kitendo walichofanya Mgambo hao kimemsikitisha “Hakuna Mfanyabiashara yoyote anayepaswa kuonewa wala kuguswa Arusha awe Mfanyabiashara wa mchicha, nyanya, Dereva wa Bodaboda au Bajaji na wengine wote”
Makonda amesema endapo maagizo yake yasipotekelezwa ndani ya saa 24 Viongozi wote wanaohusika na soko hilo atakula nao sahani moja.
Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.
0 Comments:
Post a Comment