LUKUVI MAONESHO HAYA YAWE FURSA KWA WAJASILIAMARI NCHINI


 Wazazi William Lukuvi akiwa katika banda la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru.



Taasisi zinazosimamia ama kutoa huduma za uwezeshaji wananchi kiuchumi zimetakiwa kuwashauri na kuondoa urasimu kwa wananchi ili waweze kuondokana na  changamoto mbalimbali wanazokutananazo katika harakati za kujiinua kiuchumi.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na uratibu Willium Lukuvi ametoa wito huo leo wakati akifungua rasmi maonesho ya saba ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi kanda ya kati yanayoendelea mkoani Singida.

Katika ufunguzi huo Katibu Mkuu wa Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi Beng Issa,amesema lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wananchi kujifunza na kunufaika na mikopo itakayowasaidia kukuza uchumi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewaambia wananchi wa mkoa huo kuendelea kujitokeza kwenye maonesho hayo ili kupata fursa ya kujifunza.

Hata hivyo amesema Serikali imeendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani hapo na kufanya mkoa na wananchi wake kuendelea kuimarika kiuchumi.

Maonesho ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yalianza tangu September nane mwaka huu na yanatarajiwa kufikia tamati September 14 mwaka huu ambapo yamefunguliwa rasmi leo na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na uratibu Willium Lukuvi na yameshirikisha wajasiriamali kutoka mikoa sita ya Dar es salaam,Manyara,Shinyanga,Tabora,Dodoma na Singida na ni maonesho ya saba tangu kuanzishwa kwake.



About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment