Zaidi ya shilingi bilioni 69.7 kugharamia matengenezo ya barabara mkoani Singida

SINGIDA 

WAKALA wa barabara TANROADS mkoa wa Singida,umetumia zaidi ya shilingi bilioni 69.7 kugharamia matengenezo ya barabara kipindi kilichoishia karibuni,ili ziweze kupitika kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na meneja TANROADS mkoani Singida,injinia Msama Korasoni Msama,wakati akitembelea na kukagua uboreshaji wa barabara za manispaa ya Singida.

Ameongeza kwamba  katika kuhakikisha barabara za mkoa zinapitika muda wote,wakala wa barabara-TANROADS,unaendelea na operesheni ya kukagua maeneo korofi na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu.

Injinia Msama amesema mafanikio makubwa ya uboreshaji wa barabara za mkoa,yanachangiwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassani.

“Rais wetu mama Samia anatupatia fedha za kutosha, kuhudumia barabara za mkoa wetu.Pia kusafisha/kuhudumia madaraja na vivuko vyake.Kwa ujumla miradi tunayoihudumia mingi imekamilika”,alisema na kuonge;

 “Michache iliyobaki,inakaribia kukamilika.Barabara ya Shelui-Sekenke ya kilometa 20,tutaijenga kwa kiwango cha lami,ili ipitike kwa urahisi zaidi”.

Kuhusu barabara ya kuanzia Ilongero wilaya ya Singida, hadi Hydomu wilaya ya Manyara itakayojengwa kwa kiwango cha lami,wakati wo wote kuanzia sasa,zabuni yake itatatangazwa wakati wo wote.

Katika hatua nyingine,alisema mkandarasi mzawa Janes Ezra anayemiliki kampuni ya Kangwa General supplies Ltd,ameifanyia uboreshaji barabara inayopita ziwa Kindai na ziwa Monangi,inakaribia kukamilika.Ambapo itapitika kwa urahisi”,amesema meneja huyo.

Akiongeza,Janes alisema kuwa wakandarasi wazawa kwa ujumla wameonyesha wazi  kazi wanaiweza,hivyo kilicho mbele ni serikali na wadau mbalimbali,kuwaamini na kuwapa kazi za aina yo yote.

Aidha,Janes ametumia fursa hiyo kuonya kwamba kuna uharibifu mkubwa wa barabara,unafanywa na watu wenye nia ovyo.Pia kuharibu vyuma na alama za barabarani upingwe vita.

“Watu wa  aina hii wakamatwe na kufikishwa mbele ya mahakama.Huko  wachukuliwe hatua stahiki,zitakazowaongofya watu wengine, kufanya uharibifu”,amesisitiza.

Naye injinia Majengo wa kampuni ya Jam engineer’s co,ltd,amewataka wakandarasi wenzake wazawa,wawe makini zaidi kutekeleza kazi wanazopewa, ili waaminike na  serikali na  wadau wengine.

“Rasi wetu mama Dk.Samia,anatupa fedha nyingi na kwa wakati,sisi tulipe kwa kufanya kazi kwa kiwango kinachoaminika, na wakati unaopangwa”,amesisitiza.

Ametoa wito kwamba miuondo mbinu ya barabara  itunzwe na kulindwa, na wananchi wasivamie maeneo ya barabara.

Amesema kuwa TANROADS inatambua wazi kuwa barabara ni muhimu kwa vile zinaunganisha watu.Hivyo ni farari kwetu kuzitunza.

About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment