Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema makundi ya wapiganaji katika mataifa kama vile Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo, Myanmar, Ukraine, Sudan na Ukanda wa Gaza yanapuuza sheria za kimataifa.
Antonio
Guterres ametoa wito kwa viongozi kujitolea kwa ajili ya amani na
usalama duniani kote na kuheshimiwa kwa haki za binadamu.
Akizungumza wakati wa kikao chake cha kwanza cha baraza la haki
za kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Katibu Mkuu huyo
ametahadharisha kuwa hali ya usalama inazidi kuwa mbaya duniani.
Ameongeza kuwa, mizozo duniani inawasababishia watu mateso
makubwa na haki zao binadamu kutoheshimiwa.
Guterres pia amelitetea shirika la Umoja wa Mataifa la
kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, akilitaja kama uti wa mgongo kwa
juhudi za usaidizi katika ukanda wa Gaza wakati
linakabiliwa na shinikizo la kutaka kuvunjwa.
"Moja ya ahadi ya ulinzi ya mashirika yote ya Umoja wa Mataifa
ni kufanya kila linalowezekana kulinda watu."
Naye Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu
Volker Türk ametahadharisha kuwa kazi ya chombo hicho iko hatarini kutokana na
kile alichokiita kuwa "majaribio ya kuendelea kudhoofisha uhalali na kazi
ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine".
0 Comments:
Post a Comment