SINGIDA
Jumla ya wahitimu 548 kutoka kampasi za Dar es Salam,Mtwara,Zanzibar,Kigoma na Singida,ikiwa wanawake 264,na wanaume 284 wametunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali za masomo ikiwemo shahada ya uzamili, astashahada na astashahada katika fani mbalimbali katika chuo cha Uhasibu kampasi ya Singida.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika mahafali ya wanafunzi hao kutunukiwa shahada ya Uzamili tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 24 katika Chuo cha Uhasibu ambapo amewaasa wahitimu kwenda kuwa kioo cha maadili na mfano wa kuigwa katika jamii zao.
Amesema wahitimu hayo wanatakiwa kutofumbia macho maovu yanayofanyika ikiwemo Rushwa,na matumizi ya madawa ya kulevya.
Dendego amesema wahitimu hao ni miongoni mwa watu wanaotegemewa katika kuteleza ilani ya chama cha Mapinduzi pamoja na dira ya Taifa.
Kwaupande wake Mtendaji mkuu wa TIA prof,William Pallangyo amesema maarifa waliyoipata ikatoe majibu ya changamoto zinazowakabili wananchi kwani ufanisi wao haupo kwenye vyeti walivyopewa bali ujuzi walioupata.




0 Comments:
Post a Comment