RPC KAGERA, OCD BUKOBA, GAVANA BWANKU WAFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA KATA YA KATORO

 





*RPC KAGERA, OCD BUKOBA, GAVANA BWANKU WAFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA KATA YA KATORO.*

_RPC asikiliza kero za wananchi, ahamasisha ulinzi shirikishi, kutunza amani na kupinga uhalifu._

Tarafa ya Katerero hakuna Jumamosi wala Jumapili, Kazi Inaendelea hadi Wikendi kuhudumia wananchi. Leo Jumamosi Juni 14, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera (RPC) Afande Blasius Chatanda amefanya Mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Kata ya Katoro ndani ya Tarafa ya Katerero Wilayani Bukoba. 

Mkutano ulijikita kusikiliza kero za wananchi na kuendelea kuhamasisha wananchi kulinda amani kwenye maeneo, kuhamasisha ulinzi shirikishi, kupinga na kuripoti uhalifu hasa nyakati hizi Taifa likijiandaa kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu. 

RPC Chatanda aliongozana na timu yake ya mkoa, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Bukoba (OCD) Afande Marwa Mwita, Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku, Viongozi wa CCM, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.

About MWESI MEDIA

Asante Mfuatiliaji wa Mwesi Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi 0757 056 462 Asante na Endelea Kubaki nasi.

0 Comments:

Post a Comment